IT awaandikia ujumbe kupitia Instagram chama cha wasanii Zanzibar (Z.F.U)

0

Msanii wa muziki wa kizazi kipya Iddi Thabit a.k.a IT baada ya kujitoa katika chama cha wasanii wa muziki kizazi kipya Zanzibar (Z.F.U) hivi karibuni ameonekana kukasirishwa na baadhi ya vitendo na kuamua kuwaandikia ujumbe mzito kwa chama hicho.

IT

Kupitia akaunti yake ya Instagram I.T anasema kuwa kisa cha kujitoa katika chama ni kutokana na uongozi mbovu pamoja na wasanii wachanga kutopewa nafasi kushirikia katika shuhuli za chama hicho.

Soma ujumbe huo:

1.MIMI SINA BIFU NA CHAMA CHA WASANII ZANZIBAR (Z.F.U),

2.MIMI SINA BIFU NA WANA CHAMA WA Z.F.U.

3. MIMI JINA LANGU LIPO KABLA Z.F.U.

4. MIMI SILIPWI NA Z.F.U.

5. WALA HAINA MSAADA KWANGU ZFU.

6. MIMI NDO NILIE PIGA KIFUA Z.F.U IKAWA NA EQUIPMENT ZAKE NA OFISI YAKE.

7. MIMI NIMEJIOTOA KWAKUA NIMEONA UONGOZI ULIOPO HAUFAI WALA HAUNA UCHUNGU NA MZIKI WA ZANZIBAR.

8. LAZIMA ITAMBULIKE KUNA WASANII WADOGO HAWATAKI KUWAPA NAFASI WAMEKUA WAKIITANA KWA KUJUANA BILA KUWASHIRIKISHA WALE WASIO NA MAJINA KWANINI??? 9. NATAKA IKUMBUKWE KUA KAMA MIMI WANGELI NIBANIA HAWA NINGEKUWA WAPI..?? CHUCHU.
G.LOVER.
RAMA B.
DJ.SALEH.
DJ.K
DJ.SAM
BLACK MASTER
SISTER WINNY
COOL T
DJ.MAHAJ
BUJU MANDEVU.
COOL B.
COOL PARA.
HAS J.

MKITAKA MSITAKE LAZIMA MUEKE AKILI ZENU VIZURI NA MTAMBUE KUA HICHO NI CHAMA CHA WASANII WA ZANZIBAR NA SIO WATU FULANI…UWONGOZI HAUFAI LAZIMA2 UBADILIKE NA UJUE KUA KUNA WASANII UNDER GROUND WANAHITAJI MSAADA NYINYI HAMUWAPI. WAUPATE WAPI???
ANGALIENI KWA KUHAKIKISHA TENA KWA USHAHIDI HASA MSANII GANI MDOGO MMEMCHUKUA KATIKA WIMBO WA MAPINDUZI??? SI NDO WALE WALE.. AGH.

10. SI KILA MFANYA KAZI AWEMO KWENYE CHAMA CHA WAFANYA KAZI…. NINA HOJA NA POINT ZA MSINGI DHIDI YA (ZFU) CHAMA CHA WASANII WA MUZIKI WA KIZAZI KIPYA ZANZIBAR.
NI MWANA CHAMA HALALI NA USAJILI NIMEKAMILISHA HIVYO NIMEAMUA KUA MUASI DHIDI YA UWONGOZI WA KIDIKTETA DHIDI YA WASANII WADOGO. UNDERGROUND.

AHSANTENI… BY IDDI THABIT (I.T).