Categories
Videos

Video: Fid Q Feat. Taz – Walk It Off

Farid Kubanda ambaye wengi tumemzoea kwa jina la Fid Q kaja na video mpya ya Walk It Off kamshirikisha Taz, mkali wa mashairi kaja na video ambayo unaweza kuita moja kati ya video bora za wasanii wa Tanzania kwa mwaka 2016. Enjoy video mpya ya Fid Q

Categories
E! News

Meek Mill ahukumiwa miezi 3 kifungo cha ndani ya nyumba

Meek Mill hatoenda jela lakini hatokuwa huru pia. Siku ya Ijumaa (Feb 5) hakimu aliyesimamia kesi ya rapa huyo kutokea Philadelphia aliamuru atumikie kifungo cha miezi 3 akiwa nyumbani kwake kutokana na kesi inayomkabili.

Mtandao wa TMZ ulieleza kuwa, Meek Mill hukumu hiyo aliyopewa ya kutumikia siku 90, atashindwa kufanya show zake, kutengeneza nyimbo mpya na wala kutengeneza nyimbo za uchokozi. Vile vile hakimu Genece Brinkley aliongezea hukumu nyingine ya kukaa katika kifungo cha majaribio kwa muda wa miaka sita.

 

Categories
Sports

Picha: Ligi kuu Zanzibar, Zimamoto na Kijichi

Ni mechi iliyofanyika uwanja wa Amani, Zanzibar. Katika mechi hiyo iliwakutanisha vijana wa Zimamoto na Kijichi ambapo timu ya Zimamoto iliondoka na ushindi wa goli 1 kwa bila.

image image image image image image

Categories
Sports

Valencia wafungwa 7-0 na Barcelona

Klabu ya Valencia chini ya nyota wa zamani wa Manchester United Gary Neville ilipokezwa kichapo cha mwaka na klabu ya Barcelona katika nusufainali ya michuano ya Copa del Rey baada ya kufngwa magoli saba
Mechi hiyo ya mkondo wa kwanza ilichezewa uwanjani Nou Camp.
Luis Suarez alifunga mabao manne, huku nyota wa Argentina Lionel Messi naye akijizolea magoli matatu.
Neymar alishindwa kufunga penalti.
Valencia walidhofishwa zaidi na hatua ya beki Shkodran Mustafi kumchezea visivyo Messi kipindi cha kwanza, kosa lililomfanya kufukuzwa uwanjani.

Categories
Videos

Video: Timbaland Feat. Mila J – Don’t get no betta

Timbaland and Mila J are out to prove that it “Don’t Get No Betta” in the video for their collaboration off Timbo’s mixtape King Stays King. The R&B siren strips down to lingerie in the sultry visual (via The FADER), while Timbo puts the moves on his sexy co-star. Their chemistry reaches a peak when Timb runs an ice cube up and down Mila’s body.

Categories
Music

Music: Temba Feat. Jokate & Yamoto Band – Fundi

Wimbo mpya wa Temba akiwa amewashirikisha Yamoto Band na mwanadada Jokate (Kidoti), jina la wimbo ‘Fundi’ uliofanywa chini ya producer Marco Chali katika studio za MJ Records

http://www.audiomack.com/song/zenji255/fundi

 

 

Categories
Music

Music: Ali Kiba – Lupela

Baada ya wimbo wa “Nagharamia” kutoka kwa Nyota wa muziki wa Bongo fleva maarufu kama Alikiba, hapa tumekuwekea wimbo mpya wa Nyota huyo unaitwa “Lupela” take your time to enjoy the new music hapa.

http://www.audiomack.com/song/zenji255/lupela

 

Categories
Music

Music: Mantuzzo feat. Barnaba – Furaha yangu

Msanii kutoka kusini mwa Tanzania ambaye anayefanya kazi zake visiwani Zanzibar Mantuzzo, amefungua mwaka kiaina yake na wimbo mpya ‘Furaha Yangu’ akiwa amemshirikisha Barnaba. WImbo umefanywa na producer Aloneym katika studio za High Table Sound. Sikiliza hapa

http://www.audiomack.com/song/man-tuzzo/furaha-yangu

 

Categories
Z! Extra

Tamasha la ZIFF limetoa maombi ya kushiriki

Tamasha la nchi la Majahazi ZIFF ni tamasha kubwa la filamu, Muziki na Sanaa hapa Afrika Mashariki ambalo hukusanya watu mbalimbali kutoka katika pamde zote za dunia. Katika tamasha la ZIFF unaweza ukaona kama Muziki kwa 100% ‘live’ kabisa ambalo huburudisha wakazi wa Zanzibar kwa muda siku 10.

Kwa mwaka 2016 tamasha la ZIFF lishaanza kutoa maombi ya kushiriki katika tamasha hilo kwa wasanii wa muziki na bendi zote zinazofanya muziki wa aina mbalimbali. Mwisho wa kukusanya maombi haya ni 31 Machi, 2016

Kushiriki katika tamasha hilo bonyeza hapa kwa maelekezo zaidi http://www.ziff.or.tz/callforartists2016/

Categories
Photos

Picha: Wakushi, Baby J na Rico Single katika ‘live’ show

Kama ulipitwa na wikiendi iliyopita basi hii hapa nakusogezea karibu angalia jinsi show ya Wakushi, Baby J na Rico iliyofanyika Jambo Beach Bungalows, Paje.

53 2 1 7 8 9 10 11 12 13 14 5 6

Categories
Sports

Picha: Ligi kuu ZNZ,Mafunzo na Black Sailors

Ligi kuu ya visiwani Zanzibar bado inaendelea kuwaka moto katika uwanja wa Amani, ambapo timu mbili kati ya Mafunzo na Black Sailors zilikutana. Katika mechi hiyo Black Sailors waliondoka na furaha baada ya kushinda goli 3 na kuwafanya timu ya Mafunzo kuondoka bila ya kushinda hata goli moja.

1 2 3

 

Categories
Z! Extra

Kanye West na Wiz Khalifa wamaliza ugomvi wao

Kila kitu sasa kimesuluhishwa kati ya Kanye West na Wiz Khalifa. Ni baada Kanye kuandika katika ukurasa wake wa Twitter kuwa:

https://twitter.com/kanyewest/status/694620226743238656

Beef hiyo ilimalizika baada ya mke wa Kanye, Kim Kardashian kuonekana katika ‘selfie’ ya pamoja na ex wa Wiz Khalifa, Amber Rose.

kim-amber

Categories
Sports

Picha:Ligi daraja la kwanza Taifa Jan’gombe na Idumu

Picha: Zanzinews

_MG_0934

Kikosi cha Timu ya Taifa ya Jangombe wakipasha misuli kabla ya mchezo wao na Timu ya Idumu ya Unguja Ukuu kuwania nafasi ya kushiriki Ligi Kuu ya Zanzibar kwa mwaka ujao mmchezo uliofanyia usiku uwanja wa Amaan Zanzibar

2

Wapenzi wa Timu ya Taifa ya Jangombe wakiishangilia Timu yao wakiwa jukwaa la Urusi.

3

Kikosi cha Timu ya Idumu ya Unguja Ukuu wakipasha kabla ya mchezo wao na Timu ya Taifa ya Jangombe uliofanyika uwanja wa Amaan jana Usiku.

4

5

6 7

8 9 10

Categories
E! News

Rose Ndauka Azindua Jarida lake ‘Rozzie’

Na Dotto Mwaibale
MSANII wa filamu Tanzania, Rose Ndauka  amezindua jarida  jipya liitwayo Rozzie litakalotoka  mara moja kwa kila mwezi.
Akizungumza jijini Dar es Salaam juzi, wakati wa uzinduzi huo, Rose alisema dhumuni kubwa la jarida hilo ni kuelimisha, kuiburudisha, kuikosoa na kuichochea jamii katika kufikia malengo yao ya kimaisha  kwa ujumla  na kujenga taifa bora lenye maendeleo.
3
“Pia katika kurasa za ndani  za jarida hilo  zipo kurasa zilizobeba mambo ya fasheni, maisha pamoja na mambo mbalimbali yanayoikosoa jamii pale inapokosea,” alisema.
Alisema kuwa lengo la kutoa jarida hilo ni kuwafikia watanzania wote na nakala yake itapatikana  kwenye mtandao ya kijamii mara moja kwa kila wiki.
Alisema magazine hiyo anaitoa bure  kwa watanzania wote  na litakuwa likitoa taarifa  taarifa mbalimbali  kwenye mitandao yote ya kijamii ambayo ni Facebook, Instagram, Twitter na You Tube.
2
Meneja  wa jarida la Rozzie, Ramadhani Mwanana, alisema wameanza kwa kuchapisha kopi 5,000 na jinsi wanavyoendelea waziongeza  nyingi zaidi.
Alisema jarida  hilo ltasambazwa katika mikoa yote hapa nchini  kwa kutumia magari makubwa ya mikoani, maduka mbalimbali pamoja na nyingine zitakazowezesha watanzania kupata magazine hiyo.
Categories
Videos

Video: Navy Kenzo – Kamatia

Video mpya ya Navy KenzoNahreel na Aika’ imetayarishwa na muongozaji wa video kutoka Afrika kusini Justin Campos wa kampuni ya Gorilla Films. Wimbo ni ‘Kamatia’ na video na audio zote zimetoka January 30, 2016 kama suprise kwa mashabiki wao.

 

Categories
Z! Extra

Kanye west ‘Sitozungumzia tena kuhusu watoto’

Kanye West ameomba radhi kwa Amber Rose naWiz Khalifa baada ya kumuongelea vibaya mtoto wao Sebastian kwenye twitter yake hivi karibuni.

Kanye hakuomba msamaha wa moja kwa moja bali aliandika kwenye Twitter

https://twitter.com/kanyewest/status/693276838320189440

Hayo yalitokea baada ya Kanye kuandika katika ukurasa wake na kumwambia Wiz Khalifa “You wouldn’t have a child if it wasn’t for me,”  Aliandika West (38) aliendelea kusema “You own waves???? I own your child!!!!”

Categories
Z! Extra

Avunja rekodi kwa kukaa masaa 121 akiangalia filam

Johannesburg: Raia mmoja wa Canada anaeishi South Africa amepata umaarufu mkubwa baada ya kuvunja rekodi iliyowahi kuwekwa hapo mwanzo kwa kukaa masaa 120 na dakika 23 bila ya kulala, na kuiandika rekodi hiyo upya kwa kutumia masaa 121 na dakika 18 akiangalia filamu.
Suresh Joachim, aliyevunja rekodi hiyo kwa kuongezea saa moja na kuweka rekodi mpya katika vitabu vya Guinnes World Records. Alisema ana furaha sana kuwemo katika rekodi za Guinness akiwa Africa.
Kabla ya Joachim kuvunja rekodi hiyo, Ashish Sharma kutoka India alivunja rekodi hiyo kwa kuangalia filamu 48, kwa masaa 120 na dakika 23.

Categories
E! News

Diamond ashinda tuzo nyingine

Mmiliki wa hit song ya ‘Utanipenda‘ Diamond Platnumz amezidi kuziandika headline katika ulimwengu wa sanaa baada ya usiku wa leo kuzinyakua tuzo mbili za Hipipo Awards zilizofanyika Uganda.

Ushindi alioupata ni Nyimbo bora Afrika Mashariki na Video bora Afrika Mashariki ambazo zote ni kupitia wimbo wa Nana.

Baada ya ushindi kupitia account yake ya Instagram Diamond aliandika maneno haya

View this post on Instagram

Wow! Realy wanna Thank GOD for keep blessing the innocent kid… also wana thank all Media and My Loyal fans for the Big love.. Two Awards tonight on @HipipoAwards UGANDA…EAST AFRICA SUPER HIT #NANA and EAST AFRICA BEST VIDEO #NANA many thanks to my brother @2niteflavour @i_am_godfather and all Behind this Hit!!!… thanks alot @HIPIPOAwards for keep supporting the real African talent! (Wadau kijana wenu nimefanikiwa kushinda tunzo mbili Usiku wa leo kama NYIMBO BORA AFRICA MASHARIKI #NANA na VIDEO BORA AFRICA MASHARIKI #NANA nawashkuru sana kwa kura na support zote mnazoendelea kunipa….. tafadhali nisaidieni kuhesabu ni tunzo ngapi tumechkua tangu Mwaka 2016 uanze? ) shukran sana @tommyleeafrica kwa kuiwakilisha vyema @Wcb_wasafi Uganda!

A post shared by SIMBA..!🦁 (@diamondplatnumz) on

 

Categories
E! News

Drake kuachia albamu yake mwezi April

katika kipindi cha Saturday’s episode katIka Radio ya OVO Sound Radio, Drake atangaza mwezi wa April kuachia albamu yake iliyokuwa ikisubiriwa kwa muda mrefu ‘VIEW FROM 6’.

“Mimi na uongozi wangu tunajitahidi kuweka kila kitu sawa na najua itakuwa tu. Na albamu yenyewe itakuja April 2016, kwahiyo 416, nadhani utakuwa unajua nilipotokea” alisema. Katika kumbukumbu 416 ni namba ya mji wa Toronto Drake anapotokea

“Nitakupa tarehe baadae. Kwa sasa, fahamu tu kwamba tupo katika matengenezo, na tupo tayari kwa kila kitu.

Katika nyimbo zilizomo katika albamu yake, ameachia wimbo mpya inayoitwa ‘SUMMER SIXTEEN’ iliyotengenezwa Noah ’40’ Shebib, Boi-1dana Cubeatz.

“Naangalia mbele kuwapa mtazamo wangu wote hivi karibuni” Alimaliza kwa kuwaambia mashabiki wake

View this post on Instagram

@ovo40

A post shared by champagnepapi (@champagnepapi) on

Categories
Sports

Pato na Miazga waanza mazoezi rasmi Chelsea FC

Wachezaji wapya Alexandre Pato and Matt Miazga Walionekana wakifurahia siku yao ya kwanza mazoezini katika mji wa Cobham tangu wajiunge na klabu ya Chelsea.

Wachezaji hao walimaliza maelewano ya kujiunga na klabu hiyo siku mbili zilizopita na kuwaona wachezaji wenzao na kuanza nao mazoezini Kwa ajili ya mechi kati ya MK Dons hapo kesho (Jumapili).

Miazga

Matt Miazga (20) ambaye ni mlinzi wa kati amesaini mkataba na Chelsea kwa Miaka minne na nusu.

Alisema: ‘Nina furaha na kujiunga na Chelsea, klabu maarufu duniani na yenye mafanikio makubwa. Nina furaha kuwemo katika ligi ya Premiere, ligi bora duniani na nitafurahi sana nitakapo onana na wachezaji wenzanguna kuendelea na majukumu mengine’.

Pato

Pato, ni mshambuliaji anayeongoza kuwa na uchezaji mzuri anapokuwa uwanajani. Mchezaji amejiunga klabu ya Chelsea kwa mkopo akitokea timu Corinthians ya Brazil. kabla ya hapo, mwaka 2013 Pato aliondokankatika klabu ya Milan akiwa na magoli 63 na kushiriki mechi 150.