Categories
Z! Extra

Mtandaoni: Mchungaji atoa maombi akiwa juu ya waumini wake (Picha)

Kutoka mtandaoni hivi karibuni ilivuma stori ya mchungaji hapa Tanzania, ambaye akifanya maombi akiwa juu ya migongo ya waumini au amebebwa huku akiendelea kutoa maombi kanisani hapo. ANGALIA

mchungaji1 mchungaji2 mchungaji3

Categories
E! News

Stori: Wimbo wa Nay wa Mitego ‘Shika Adabu yako’

Nay wa Mitego Leo ameachia ngoma yake mpya inayoitwa “shika adabu yako”ambayo kama kawaida yake amewachana watu wengi ndani ya mistari yake.
Mwaka uliopita ROMA alitoa wimbo wa VIVAROMAVIVA Ambao ulifungiwa pamoja na nyimbo nyingine na BARAZA LA SANAA TANZANIA (BASATA) kwa madai kuwa aliwasema Watu kwa maneno yasiyo na ushahidi. HUENDA NAY AKAPITIWA NA WEMBE HUO?
Mapema Leo amefunguka kuwa kabla ya BASATA kuufungia itabidi wajitathimini kwanza kwasababu hata wao ni moja ya Watu waliochanwa humo ndani.
Mistari inayowalenga BASATA ndani ya ngoma hiyo inasikika nay akiwatupia lawama kwa kufungia wasanii bila mpango.
Nay amepost kwenye ukurasa wake wa Instagram kuwa baada ya ngoma hii atapumzika na tayari ameshasema itakuwa mwezi mmoja tu.

Soma Alichokiandika

 

LENGO LA WIMBO HUU.
Nay amesema ameamua kutoa ngoma hii kwasababu muda mrefu game haijachangamka na hakuna aliyetoa ngoma ya kuleta challenge baina ya Watu kwahiyo ameileta hii  kuchangamsha genge. SIKILIZA HAPA WIMBO MPYA WA NAY

http://www.audiomack.com/song/zenji255/shika-adabu-yako

 

Categories
E! News

Alichokiandika Diamond kwa Mashabiki wake

Star wa Bongo fleva na mmiliki wa hit song ya ‘Utanipenda’ Diamond Platnumz asema habari mpya na kama wewe ni shabiki wake basi soma ujumbe aliokuwekea kupitia account yake ya Twitter na kuandika maneno haya.

 

Categories
E! News

Stori 2: Drake hatotumbuiza Tuzo za Grammy na Rihanna kuja Afrika Mashariki, June

Drake hatotumbuiza katika tuzo za Grammy, Marekani

Onyesho kubwa la utoaji tuzo lenye kuhusisha mastaa mbalimbali wa filamu na muziki huko marekani la Grammy, kwa mwaka huu Drake hatofanya onyesho kama hapo mwanzo ilivyoelezwa. Drake aliandika mwenyewe kwenye ukurasa wake wa Twitter

‘ sitofanya onyesho katika tuzo za Grammy…’

Rihanna kutumbuiza Afrika Mashariki, June 2016

image

Rihanna anatarajia kukanyaga ardhi ya Afrika Mashariki, June mwaka huu.

Mrembo huyo anatarajiwa kutumbuiza nchini Uganda. Ziara yake imeandaliwa na promota maarufu wa nchini humo, Suudiman Lukwago. Hiyo itakuwa ni mara ya pili kwake kuja Afrika baada ya mwaka 2013 kutumbuiza nchini Afrika Kusini.

Taarifa hizo zilisambazwa na mkurugenzi wa kampuni ya ulinzi aitwaye Dixon Okello aliyeandika:

“Just signed a deal with top international promoter Suudiman Lukwago to handle event security during the Moses Golola Vs Titus Tugume non-title super middleweight kick boxing fight on the 14th Feb 2016 at the MTN arena Lugogo and international Diva Rihanna concert in June. I have handled most international kickboxing fights and concerts in the past and hope all will be well.”

Chanzo: Bongo5.com

Categories
Newspapers

Simu TV: Vichwa vya habari Magazetini leo tar 9

Kupitia mtandao wa Simu TV nakuletea Stori zote kubwa zilizobebwa kwenye Magazeti ya Tanzania kuanzia kwenye Siasa, Michezo na hardnews ili ujue kinachoendelea.

 

Categories
Sports

Picha: Ligi Kuu Zanzibar, Kimbunga na KMKM

Ni mechi iliyofanyika uwanja wa Amani, Zanzibar. Katika mechi hiyo iliwakutanisha vijana wa Kimbunga na KMKM ambapo timu ya Kimbunga iliondoka na ushindi wa goli 1 kwa 0.

2 3 4 5

Categories
E! News

Nuh Mziwanda asema Shilole anamfanyia fitna ashuke kimziki

Baada ya kuvunjika kwa mahusiano yao aliyekuwa mpenzi wa SHILOLE, Nuhu Mziwanda amesema Ex wake huyo anamfanyia fitna ili kumshusha kwa kumharibia kisanaa.
Mziwanda amesema sasa ndiyo amegundua kuwa Shilole alikuwa kwake kimapenz tu na hakuwa na urafiki wowote na ndiyo maana anadiriki kufanya hivyo Siku chache tu baada ya kuachana.
Akifafanua zaidi amesema Shilole ameingia kwenye account yake ya Instagram na kubadilisha password kiasi kwamba licha ya kujaribu kwa wataalamu wa teknolojia bado hajaweza kuirejesha.
Pia amesema Shilole amekuwa akisambaza maneno ya kashfa kwa watu wake wa karibu ili kumharibia sifa yake na kumpotezea mashabiki.
Nuhu amefuta Tatoo ya Shilole na amesema amefanya hivyo baada ya kugundua mtu mwenyewe kumbe hamtakii mema.
KUHUSU PENZI JIPYA.
nuhu amesema tayari ameshapata mpenzi lakini amejifunza mambo ya mapenz siyo ya kuyaanika mitandaoni na amegundua ule ulikua utoto na sasa hawezi kurudia tena.

Categories
E! News

Fahamu: Sababu ya Fid Q kuandika verse fupi katika WALK IT OFF

Baba lao FARID KUBANDA ,FID Q amesema sababu iliyofanya kuchana verses fupi fupi kwenye ngoma yake mpya #walkitoff ni kwasababu alitaka mashabiki wainjoy zaidi muziki wake na hivyo wangehitaji kitu cha tofauti.
Fid amesema ashazoeleka sana kuchana virse ndefu lakn hiyo siyo njia pekee ya kuwateka mashabi kwasababu kwenye KIMOSABE alichana sana lkn mashabiki kama wakakaza hivi kwahiyo this time ameamua kuja kivingine.
Fid ametoa video ya ngoma hiyo na imekuwa ikisifiwa sana na RAIA kua amekuja kitofauti laki SAFIII.
Ameahidi video nyingine kibao zinakuja

Categories
E! News

Adam Juma ameyaandika haya baada ya kuitazama video mpya ya Ali kiba ‘Lupela’

Siku moja baada ya staa wa bongofleva Ali kiba kuiachia video ya ngoma yake ‘Lupela‘, leo Director wa long time Tanzania Adam Juma ameyatoa yake ya moyoni kupitia account yake ya instagramn baada ya kuona comments za watu wengine wakiikosa video yenyewe.

Baada ya kuandika hayo director baadae alirudi tena na kuandika maneno ambayo yanaonekana kuna baadhi ya mashabiki au wasanii hawajapenda kwa kile alichokiandika kuhusu video ya Ali Kiba.

 

Categories
Videos

New Video: Jumaa Town ft. Maromboso – Mpambe

Mpambe ni wimbo kutoka kwa kijana anaefanya shuhuli zake za muziki katika visiwa vya Zanzibar. Jumaa Town akiwa amemshirikisha kijana kutokea Yamoto Band, Maromboso amesimama kwenye kiitikio. Audio imefanywa katika studio Island Records Zanzibar na video imetengenezwa na Director Minzi Mims. Muone mpambe akifanya yake.

 

Categories
Newspapers

Simu TV: Vichwa vya Habari Magazetini leo tar 8

Kupitia mtandao wa Simu TV nakuletea Stori zote kubwa zilizobebwa kwenye Magazeti ya Tanzania kuanzia kwenye Siasa, Michezo na hardnews ili ujue kinachoendelea.

Categories
Videos

Video: Ali Kiba – Lupela

Ni siku mbili zimepita toka Ali kiba alipoifanya party ya kuitambulisha video yake mpya kwa Watanzania wachache waliopewa kadi za mwaliko, ila sasa hivi ameiachia video kwenye Youtube ili kila mtu aitazame… ni video ambayo aliifanya Marekani wiki kadhaa zilizopita….

Categories
Sports

Ligi kuu Uingereza kati ya Chelsea na Man Unite

Ligi Kuu Uingereza imeendelea tena leo February 7 kwa michezo miwili kupigwa, AFC Bournemouth walikuwa wenyeji wa Arsenal katika uwanja wao wa nyumbani, wakati Chelsea walikuwa wenyeji wa Man United katika dimba lao la Stamford Bridge, mchezo ambao ndio uliteka hisia za mashabiki wengi wa Ligi Kuu Uingereza.

Chelsea ambao bado wapo katika kipindi cha mpito chini ya kocha wao wa muda Guus Hiddink, wamefanikiwa kutoa sare ya goli 1-1, baada ya Man United kufunga goli la uongozi dakika ya 61 kupitia kwa Jesse Lingard, wakati Man United wakiwa na matumaini ya kuondoka na point tatu, Chelsea walifanikiwa kusawazisha goli dakika ya 90 kupitia kwa Diego Costa na kufanikiwa kumaliza mchezo kuambulia kugawana point moja moja.

Kwa matokeo hayo Man United wapo nafasi ya 5 wakiwa na point 41 katika michezo yao 25 waliocheza ya Ligi Kuu Uingereza hadi sasa, wakati Chelsea wapo nafasi ya 13 na point 30 wakiwa wamecheza michezo 25.

 

 

Categories
Videos

Video: Young Killer ft. Juma Nature – Popote Kambi


Young Killer, tuliisikia tu single yake kwenye audio sana lakini good news ni kwamba katuletea hii video mpya featuring Juma Nature ‘popote kambi‘. Video imesimamiwa na director Tonee Blaze.

Categories
Newspapers

Simu TV: Vichwa vya Habari Magazetini

Kupitia mtandao wa Simu TV nakuletea Stori zote kubwa zilizobebwa kwenye Magazeti ya Tanzania kuanzia kwenye Siasa, Michezo na hardnews ili ujue kinachoendelea.

Categories
Sports

Video: Angalia Man City walivyotandikwa 3-1 na Leicester City

Timu inayoongoza katika ligi ya Uingereza, Leicester wamewashangaza wapinzani wao wa karibu katika ligi hiyo Manchester City baada ya kuwacharaza 3-1 katika uwanja wa Etihad na hivyobasi kupanda juu wakiwacha pengo la pointi sita.
Robert Huth alifungua dimba la mchezo huo kwa kona iliopigwa na nyota wa timu hiyo Mahrez na kuandika bao la kwanza kwa timu yake.
City ilitishia kusawazisha bao kwa kuvunja safu ya ulinzi ya Leicester huku mabeki wao wakionekana kutatizwa na washambuliaji wa Leicester.
Mahrez alifunga bao la pili huku Huth akifunga bao la tatu na kufanya mambo kuwa 3-0 kabla ya Sergio Aguero kuipatia City bao la kufutia machozi kunako dakika za mwisho.

 

Categories
Sports

Msimamo wa Ligi kuu Zanzibar

Msimamo wa ligi kuu ya Zanzibar umetoka na timu ya JKU inaonyesha kushika nafasi ya kwanza na kufuatiwa na Zimamoto ambapo nafasi ya mwisho timu ya Mtende ndio imefunga orodha hiyo ya ligi kuu.

 

POS TIMU P W D L GF GA GD PTS
1 JKU 12 10 1 1 26 8 18 31
2 ZIMAMOTO 13 7 4 2 20 8 12 25
3 B/ SAILOR 13 6 3 4 15 14 1 21
4 KMKM 12 5 5 2 16 11 5 20
5 KVZ 13 6 2 5 13 15 -2 20
6 MIEMBENI 11 5 2 4 11 12 -1 17
7 JANG’OMBE 12 4 4 4 15 15 16
8 MAFUNZO 13 4 6 3 12 10 2 18
9 KIPANGA 12 3 6 3 8 9 -1 15
10 KIJICHI 13 2 8 3 11 13 -2 14
11 CHUONI 13 4 2 7 13 19 -6 14
12 KIMBUNGA 12 3 2 7 19 19 11
13 POLISI 12 1 4 7 9 14 -5 7
14 MTENDE 13 1 3 9 6 27 -21 6
Jumla ya mabao 194 yameshafungwa kupitia michezo 87

 

Categories
Videos

Video: Steve RnB – Listen

Video ya wimbo mpya wa Steve RnB unaoenda kwa jina la Listen imefanywa na Director Joowzey na audio imefanywa na producer Mbezi. Iangalie kwa mara ya kwanza

Categories
Newspapers

Simu TV: Vichwa vya Habari Magazetini

Stori zote kubwa zilizobebwa kwenye Magazeti ya Tanzania kuanzia kwenye Siasa,  Michezo na hardnews ili ujue kinachoendelea.

Categories
E! News

Six Records yatoa ofa kwa wasanii chipukizi

Baada ya kukaa kimya na kujipanga upya kwa kipindi kirefu, studio inayopatikana pande za Mwera Six Records chini ya usimamizi wa producer Side2the Lee, Wametoa ofa kwa wasanii wanaochipukia katika fani ya muziki wa kizazi kipya (Bongo au Zenji Fleva). Side2theLee alisema kuwa katika ofa hizo itakuwemo, kurekodi wimbo mmoja bure kwa wimbo ambao utakaoridhiwa na uongozi wa studio hiyo, Kufanya video ya wimbo wake kwa gharama ya chini kabisa na kuwasaidia wasanii ambao hawawezi kutunga pamoja na upangiliaji katika sauti.

Kwa mawasiliano zaidi wasiliana na uongozi wa studio za Six kwa kupiga nambari +255 714 249 514.