Audio: Kala Jeremiah aongea kuhusu ‘Wanandoto’ ilivyorudisha furaha ya mama na mtoto wake

0

Video ya wimbo ‘Wanandoto’ ya msanii wa muziki wakufoka, Kala Jeremiah imefanikisha kurejesha furaha ya familia moja ambayo ilipotelewa na mtoto wao wa kiume toka September 2015.

kala jeremiah
Mtoto Adam aliyezungushiwa duara akiwa mmoja ya washiriki wa video ya Wanandoto

Mama wa mtoto huyo aitwae Adam, alifanikiwa kumuona mwanae huyo kupitia video ya wimbo huo ambao unazungumzia mazingira magumu wanayopitia watoto yatima.

mama-na-mwana-adam

Akizungumza na Zenji255 Kala alisema “⁠⁠⁠Nilipigiwa simu na mtu akaniambia Kuna mama kamuona mtoto wake kwenye video yangu ya Wanandoto na mtoto huyo alipotea tokea mwaka jana mwezi wa 9,” alisema Kala “Mama wa mtoto alifanya jitihada zote za kumpata mtoto wake bila mafanikio lakini juzi juzi akiwa anatazama video ya Wanandoto akamuona mwanae kwenye video na kupata mshangao na mshituko ndipo alipoamua kumtafuta mtangazaji flani wa redio flani ndipo mtangazaji huyo akanitafuta na kuniunganisha na mama huyo,”

Msikilize Kala Jeremiah akiongea kwa njia ya simu