AT ataka watu wazifanyie kazi akili zake kwani zina uwezo mkubwa kufikiri

0

Msanii wa muziki wa Mduara AT, amewataka watu kutumia akili zake na kumuweka katika vitabu vya kumbukumbu, kutokana na uwezo wake mkubwa wa kufikiri.

A.T

AT amesema iwapo msanii atafanya kitu cha tofauti na kuonyesha ulimwengu utofauti wake na bado watu wakamuelewa, haina sababu ya kutokubali kumsifia.

“Kuna watu wana desturi ya kutokuelewa vitu, nilizungumza na nikasema msanii mzuri sio yule mwenye lundo la macollaboration, msanii mzuri ni yule ambaye atafanya aina tofauti ya muziki na wenziwe, mi ningependa niwaambie mwenzio akifanya vizuri actualy msifie kafanya tofauti, na hii imejitokeza mfano ni wimbo wa Ojuelegba, mfano Aje, mfano mwengine ni ngoma ya Darasa, aina tofauti na muziki wanaofanya wenzio ukifanya utakuwa ni msanii mzuri”, alisema AT kwenye kipindi cha Planet Bongo ya East Africa Radio.

AT aliendelea kusema kuwa “kwa hiyo akili zangu muwe mnajaribu kuzifanyia kazi na kuziweka katika vitabu vya kumbukumbu, hizi akili sio 0 Kb, hii terabite MG au Gigabite hizi akili”, alisema AT.