Aliyekua meneja wa kundi la N.W.A Jerry Heller amefariki dunia

0

Kama unalikumbuka kundi la N.W.A ambalo lililokuwa linaundwa na wasanii kama Dr. Dre, Eazy E, Ice Cube na wengineo. Aliyekuwa meneja wa kundi hilo Jerry Heller, amefariki dunia baada ya kupata ajali ya gari siku ya Ijumaa (Septemba 2) na amefariki akiwa na miaka 75.

jerry heller

Ingawa alikimbizwa hospitalini baada ya majeraha makubwa kutokana na kugongana na gari aina ya mini-van, lakini hakuweza kufanikiwa na kufariki njiani akiwahishwa hospitali. Kwa mujibu wa mtandao wa TMZ ni wazi kuwa kifo chake kilitokana na matatizo ya afya, ajali, au yote mawili.

Baada ya kufanya kazi na Elton John, Pink Floyd, The Who, na wengineo katika miaka ya 60 na 70, Jerry aliweza kulisimimamia kundi la N.W.A kwa miaka minne katika miaka ya 1980, toka siku lilipozinduliwa. Hata hivyo, baada ya kuibuka migogoro ya mirabaha kati ya meneja huyo wasanii wawili Dr. Dre na Ice Cube kuliibuka ‘beef’ ya hadharani na kusababisha kusambaratika kwa kundi hilo.