Albamu ya Drake ‘Views’ yauza kopi Milioni 1.2 duniani ndani ya siku 6

0
drake

Drake aliiachia albam yake mnamo tarehe 29 April, na imekuwa ikimpandisha chati sana kutokana na mauzo hayo na kufanikiwa pia kuingia katika tano bora ya Marapper wanaokamata fedha nyingi nchini Marekani.

Republic records imeripoti kuwa, albamu hiyo ya Views imepakuliwa mara milioni 250 katika mtandao wa Apple Music. Na iTunes kuuzwa albamu milioni 1.2 duniani kote ndani ya siku 6. Ambapo katika mauzo yamejumlishwa na nchi ya Marekani ambayo iliuza albamu milioni 1.

Albamu ya Views ilishika No. 1 katika mtandao wa iTunes kwa nchi 95, katika chati 200 za Billboard albam hiyo itaanza rasmi kuingia kwenye chati hizo wiki ijayo.