Alatish Mabawa kumtambulisha ‘Twarity’ na wimbo wake mpya Jumatatu ijayo

0

Msanii wa muziki Alatish Mabawa kupitia lebo yake ya ‘Mabawa Classic’ Feb 20 atamtambulisha rasmi msanii mpya ‘Twarity’ ambaye tayari ameshatengeneza wimbo mpya unaoitwa ‘Kipenda Roho’ ambao ameshirikishwa Mabawa.

alatish mabawa

Akiongea na Zenji255, Mabawa amesema kuwa hadi sasa tayari ameshasaini msanii mmoja na bado na mipango ya kuwasaini wengine ambao watakuja kutangazwa siku za mbele.

Kwa upande wake amesema kuwa amechukua uamuzi huo baada ya kuona vipaji Zanzibar vinaibuka vipya kila siku.

“Zanzibar vipaji vipo vingi tu ila msaada wa kuvinyanyua ni mdogokuna wasanii wazuri mtaani. Nimeamua kuanzisha lebo ili kuwasaidia wasanii wenye vipaji kuonyesha uwezo wao, kupitia lebo yangu nataka kuleta mapinduzi. Na bado nina mipango mingine tofauti na muziki katika kuendeleza vipaji vipya vya hapa Zanzibar” Amesema Mabawa

Wimbo wa msanii Twarity umetengenezwa katika studio za Six Records na producer Side to The Lee akiwa pamoja na Chilly K.