Alatish Mabawa kuja na ‘wari wa leo’ na kuzindua albamu mpya hivi karibuni

0

Msanii Alatish Mabawa baada ya kusherehekea siku yake ya kuzaliwa wiki kadhaa zilizopita, Alatish ameamua kutoa zawadi ya ‘Birthday’ kwa mashabiki wake ambapo ataachia wimbo wake mpya ‘Wari wa Leo’ siku za hivi kaaribuni kuanzia sasa.

alatish mabawa

Akizungumza na Zenji255 Mabawa alisema kuwa anamshukuru mungu mpaka hapo alipofika na anatarajia kuja na zawadi kubwa kwa mashabiki wake kwani hivi karibuni ataachia wimbo mpya na utafuata uzinduzi wa albamu yake mpya baada ya kuachia wimbo huo.

“Katikati ya wiki hii tukijaaliwa natarajia kuachia kazi yangu ya mwisho ambayo itakayofunga albamu yangu ninayotaka kuizindua. Na wimbo unaitwa Wari wa leo, nimemshirikisha malkia wa mipasho Khadija Kopa na wimbo nimefanya katika studio za Akhenaton.” Alatish Mabawa alielezea.