Alatish Mabawa kuachia wimbo mpya ‘Leo Kesho’ Jumatatu hii

0

Msanii wa kizazi kipya Zanzibar Alatish Mabawa anatarajia kuachia wimbo wake mpya wa ‘Leo Kesho’ Jumatatu hii.

mabawaAkizungumza na Zenji255 Mabawa alielezea kuhusu ukimya wake wa muda mrefu ni kutokana na kuachia kazi mara kwa mara lakini mafanikio yalikuwa hayaonekani ndipo akaamua akae chini na kujipanga upya.

Mabawa aliongezea kuwa “Leo Kesho ni wimbo wangu mpya natarajia kuuachia Jumatatu ya wiki inayokuja (22, Agosti) na huu ni wimbo ambao wa kikubwa sana. Kwani ukiusikiliza wimbo huo utaona tofauti ya kiuandishi, uimbaji na kama itasapotiwa kwa nguvu zote basi inaweza ikapeperusha bendera ya Zanzibar.”