AT afunguka kuhusiana na Madj na watangazaji wa bongo juu ya wasanii kutoka Zanzibar

0
madj

Mfalme wa miduara anayetokea Zanzibar, AT amesema wasanii wengi wa visiwani humo wanafeli sababu madj na watangazaji wa redio wanawabania.

AT alisema kuwa wadau wa muziki inabidi wakumbuke kuwa Zanzibar ni sehemu ya Tanzania.

“Naona kuna watangazaji na Madj hawataki kuona wasanii wa Zanzibar wanakuwa wanafanya vizuri, wanaona kama msanii wa Zanzibar akifanya vizuri sifa itaenda Zanzibar na wakati wasanii wote wa bara na Zanzibar wanafanya vizuri,” amesema AT.

“Mimi naelewa kwakuwa nimeshafanya research. Wajue wote siye ni Watanzania na waangalie pia maslahi ya taifa maana hii itaenda huko mbeleni italeta matatizo. Nadhani hilo ndio tatizo hasa. Waache hiyo tabia maana ukionana nao na kuongea nao wanakupa ushauri mzuri sana ila lazima tu watambue kuwa shetani hafungwi jela.”

Source: Bongo5