Adebayor asajiliwa Uturuki kupitia dirisha dogo

0

Nahodha wa Togo na mshambuliaji wa  zamani wa Arsenal, Man City na Tottenham Emmanuel Adebayor amepata timu ya kuichezea baada ya kuhangaika kwa muda mrefu.

adebayor

Adebayor alikua nje ya Soka kwa takribani miezi 6 akitafuta timu ya kuichezea ambapo jana ikawa siku yake ya bahati kwake ambapo amesaini kuichezea klabu ya ligi kuu ya Uturuki, Instanbul Basaksehir.

Instanbul Basaksehir inayotumia uwanja wenye uwezo wa kuingiza watu elfu tatu tu inakamata nafasi ya pili katika msimamo wa ligi kuu ya Uturuki inayoongozwa na Besiktas ambapo Emmanuel Adebayor amesaini mkataba wa mwaka mmoja na nusu akitarajiwa kulipwa paundi 50,000 baada ya kodi kwa wiki.

Imetayarishwa na: Ali Khamis