Abramy amlaumu Producer Chilly K kwa kuvujisha wimbo wake

1

Msanii wa miondoko ya Zenji Fleva Abramy the Voice, ametoa lawama zake kwa Producer wa studio ya Action Music, Chilly K baada kuvujisha wimbo wake.

abramyHii imekuja baada ya nyimbo hiyo kuachiwa bila ridhaa yake. Abramy amesema kuwa huo wimbo ameufanya muda mrefu na mategemeo yake ilikuwa auachie Novemba 20.

“Nimejisikia vibaya sana tu, nimeona kama nahangaika kufanya kazi halafu mtu kazi yangu anaichukulia masihara tu, mimi nina uhakika wa wimbo wangu umevuja na Chilly K ndie aliyevujisha na sijui lengo lake ni nini” Amesema Abramy.

Aliongeza na kusema “Kawaida producer anapotengeneza wimbo hubakia studio na mimi siwezi nikafanya wimbo halafu nikaachia kizembezembe, yeye ndie anahusika.  Ni tayari kwamba nishakula hasara juu hili na sina jinsi, kikubwa kama watu wakiichagua na kutaka ichezwe basi ni ruhsa kufanya hivyo ” alimaliza Abramy.