UMISSETA kanda ya Unguja wataja kikosi chao kitakachokwenda Mwanza

0

Kocha msaidizi wa timu ya Kanda ya Unguja, Abdul wahab Dau “Mwalimu Dau” ametangaza kikosi kipya kinachotarajiwa cha wachezaji 21 kitakachokwenda Butimba Jijini Mwanza  katika Mashindano ya Umoja wa Michezo na Sanaa Shule za Sekondari Tanzania (UMISSETA), ambapo Kikosi hicha kinatarajia kuondoka Visiwani Zanzibar siku ya Jumamosi ya June 3, 2017.

umisseta

Mashindano hayo ya UMISSETA yanayotarajiwa kuanza kutimua vumbi June 6, 2017 katika Chuo cha Ualimu Butimba Mwanza, ambapo kwa mwaka huu Zanzibar itatoa nafasi mbili kwa kanda ya Unguja na kanda ya Pemba.

KIKOSI KILICHOTEULIWA

Walinda mlango: Aley Ali Suleiman (Ubago) na Ali Makame (Muembe ladu)

Walinzi: Ibrahim Abdallah Hamad (Arahman), Abdurahman Seif Bausi (Glorious), Abubakar Khamis (Bububu), Abdul aziz Ameir Khatib (Arahman), Ali Issa Omar (Lumumba),  Ahmed Mohd Shaaban (Nyuki) na Abbas Yahya.

Viungo: Amani Ali Suleiman (Kiembe Samaki), Ibrahim Faraj “Mess” (Lumumba), Haji Suleiman (JKU Mtoni), Yakoub Kiparo (Langoni), Jamali Ali Jaku “Ozil” (Kinuni) na Eliyasa Suleiman (K-pura).

Washambuliaji: Faki Kombo (JKU Mtoni), Mundhir Abdallah (JKU Mtoni), Ali Hassan (Bububu), Walid Abdi “Pato” (Mwera), Ali Mohd Seif (Tumekuja) na Ali Omar (Mwera).

Imetayarishwa: Ashura Ali