“Wimbo wa Hawalali umenipatia ‘Connection’ nyingi” – Abram The Voice

0
abramy

Na Mkali Nesta

Msanii wa mziki wa kizazi kipya Zanzibar Abramy TheVoice amesema wimbo wake wa hawalali umempatia connection nyingi za ndani na nje ya zanzibar. Akizungumza na Zenji255 abramy amesema “kwanza nashukuru sana unajua hawalali ni ngoma kubwa sana na imeniweka katika position nzuri katika mziki imenipatia¬† ‘connection’ nyingi sana za ndani na nje ya zanzibar” amesema abramy. Hata hivyo star huyo ameshindwa kuweka wazi siku gani video ya hawalali itakua tayari kwa upande mwengine abramy aliutaja wimbo anaoupa heshima kuliko nyimbo zote alizowahi kuimba “kiukweli wimbo ambao naupa heshima kubwa chakachua kwasababu ndio wimbo ulinitambulisha watu wakanifahamu” alimalizia Abramy.