50 Cent asema Tyson amejitolea kumfudisha Chris Brown kupambana na Soulja Boy

0

Ule ugomvi wa mastaa wawili kati ya Chris Brown na Soulja Boy baada ya kurushiana maneno kwenye mitandao sasa unahamia ulingoni.

50 cent

Pambano hilo lililoandaliwa na Floyd Mayweather imeripotiwa litafanyika mwezi huu ambapo mastaa wengi nchini Marekani wamevutiwa nalo.

Rapa 50 Cent kupitia akaunti yake ya Instagram amesikika akisema kuwa: “Nimemaliza kuongea na ‘Iron’ Mike Tyson kwa njia ya simu na amekubali kumfundisha Chris Brown.”

Wakati huo huo Mayweather atamfundisha Soulja Boy lakini inaonekana kuwa 50 Cent hakufurahishwa na Mayweather akiwa kama promota wa pambano hilo na kujitolea kumfundisha Soulja Boy kwani angemuachia mtu mwingine akamfundisha msanii huyo.